Mambo 2 Kutoka kwake yanayoashiria kuwa mpenzi wako ni husband material

#1 Anakufanya ujisikie na ujione mzuri ndani na nje, Hata iweje.

Kama mwanaume wako anakusifia na kukwambia wewe ni mzuri hatakama kwa muda huo unahisi hauvutii, huyo ni fundi. Kama anakufanya utabasamu muda wote, kwa sababu anajua wewe ni mzuri na mwema, bado yeye ni fundi – anafaa. Kama utakuwa na mtu ambaye anakufanya usijiamini, hali itakuwa mbaya zaidi pale unapo anza kuzeeka / kuwa mama. Kama mwanaume kweli anakupenda atakupenda kwa kila kitu ulichonacho.
Hakuna dhaifu ylako lolote litakalomfanya atoke kwako – hata syiku moja. Wote kwa sasa mnaweza mkaonekana wazuri lakini kadri umri unavyozidi kwenda, mambo yanabadilika. Kumbuka , unahitaji kuwa na mtu atakayekupenda wewe ulivyo nje na ndani, kwa mazuri yako na mabaya yako.

#2 Ni mshabiki wako mkubwa sana(Ni supporter wako mkubwa).

Kama unatoka na mwanaume ambaye anaku sapoti kwa mambo mengi, hapo ujue upo na mtu sahihi. Kama unafikia hatua ya kujaribu kitu kipya, au una mpango wa kuanza biashara mpya siku zote anakuwa makini kukusikiliza na kulisapoti wazo lako. Unapokuwa katika uhusiano unahitaji kuwa na mtu ambaye atyakufanya ujisikie furahana kukuheshimu wewe pamoja na mawazo yako.
Unapokuwa na mwanaume ambaye anakufanya usiwe na amani na kukuona wewe mjinga kwa mambo yako unayofanya au unayopanga kuyafanya. Maisha yanakuwa mafupi na magumu sana unapokuwa na mtu ambaye anakuzuzua akili yako na kuonesha kutokuwa na imani na wewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *