Jinsi gani ya kuongea na msichana bila kupungukiwa Swaga

# 1Mfanye ajue kuwa unamtaka.

Najua unajua, kuongea na mwanamke kwa mara ya kwanza siyo kama mtu anayemfata mwanamke na kumuomba watoke out. Inatakiwa iende kwa hatua, lakini licha ya hiyo hautafikia lengo. Mwanamke anahitaji kujua unamtamani/ kumpenda hata kabla hamjaongea ili aweze kukuchambua / kukufahamu / kukuchunguza(to evaluate you).

Kama utamfata mwanamke ambaye kwanza hajawahi hata kukuona ukionesha interest kwake, utaishia kumshtua tu. Na ataishia kukwambia neno ambalo mama yake alimfundisha akiwa mdogo – kwamba akikutana na mwanaume amwambie nini “Niache”.

#2 Fanya mautundu.

Baada ya kujua kuna kiumbe kama wewe duniani, anza michezo ya kichokozi. Jitahidi kuwa unamuangalia kila wakati mpaka yeye ajue unamuangalia, hii itamfanya naye awe anafanya hivyo hivyo japo hatapenda kujionesha(ila usimshangae). Sasa unatakiwa kujua, na yeye anakuangalia? je marafiki wake wanakuangalia? je wanatabasamu wakikuona?. Jaribu kujua hayo.
Hakuna haja ya kutaka kujua jinsi ya kumfata mwanamke ambaye ukimtazama anakuangalia vibaya au kwa hasira, na wakati mwingine hajali kama unamuangalia au la. Kumbuomba mwanamke kutoka nae mda mwingine huwa kama majanga kama haujamvutia, hivyo kuwa mwangalifu.

#3 Usimchomoe au kumuita kutoka mahali.

Kumchomoa mwanamke kutoka sehemu fulani mara nyingine huwa smart na ya kuvutia, lakini mara nyingi siyo njia sahihi. Jitahidi kuangalia mazingira.
Mfano kama alikua sehemu fulani, kisha akawa anaondoka unaweza mfata na kusimama mbele yake na kumuabia vitu kama ” natamani ungejua ni kwa muda gani nimekua nikitamani kuwa na muda kama huu”. au kitu kingine cha kawaida. Iwe ofisini, park ya magari au hata bar, jaribu kumuuliza swali ambalo linaendana na mazingira.

Lakini kumbuka kutumia lugha ambayo itamchanganya ka kutaka wewe uongee zaidi ili akuelewe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *